Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:52 pm

NEWS: SUGU KUIBURUZA BASATA MAHAKAMANI KWA KUIFUNGIA NYIMBO YAKE

Dodoma: Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) na mwanamuziki mkongwe wa Hip Hop Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ametangaza vita na baraza la sanaa la Taifa Basata na kuapa kutumia mawakili sita kulishtaki baraza hilo, kwa kisa cha kuufungia wimbo wake wa #219, ambayo kimsingi ni namba yake ya Magereza wakati yupo kifungoni.

Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 bungeni leo Juni 20, 2018, Mbilinyi amesema kila taasisi imegeuka kuwa polisi ikiwemo Basata walioufungia wimbo huo uliovuja, kabla ya kuutoa rasmi.

Amebainisha kuwa Basata limetoa taarifa ya kuufungia wimbo huo wakati hawajui gharama alizotumia kuutengeneza. “Wimbo umevuja wao wanatoa statement (taarifa) ya kuufungia. Hawajawahi hata kuingia studio, hawajui hata gharama. Wanataka wote tuimbe nyimbo za mapenzi,” amehoji.

Wakati akieleza hayo, Sugu alikatishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza na kubainisha kuwa anachozungumza mbunge huyo wa Mbeya Mjini si sahihi.

“Wimbo unavuja vipi wakati uko kwenye mitandao. Hata mashairi yake ninayo hapa. Nyie wenyewe mlisema Basata wanafungia nyimbo bila taarifa,”amesema.

Amesema utaratibu unataka mtunzi kupeleka mashairi ya wimbo wake Basata kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuutoa katika redio, televisheni, mitandao ya kijamii na maeneo mengine.

Akijibu taarifa hiyo, Sugu amesema hawezi kumjibu naibu waziri huyo kwa sababu ni mdogo wake lakini anachofahamu ni kwamba yeye si kama wanamuziki wengine waliofungiwa nyimbo zao na baraza hilo.

“Sitampiga mheshimiwa Spika. Lakini mimi sio kama Roma. Naiburuza mahakamani Basata wimbo umevuja mimi sijautoa bado. Nina mawakili sita nitawaburuza mahakamani ndio watakoma,”amesema. Taarifa ya Basata inasema imefikia hatua hiyo kwa kuwa una maneno ya uchochezi na kuhatarisha amani na utangamano miongoni mwa jamii. Mbali na kuufungia Basata pia imetoa onyo kwa msanii huyo kuutangaza na kuusambaza kwa watu wengine.

Katika wimbo huo wenye beti tatu, mbunge huyo anazungumzia harakati zake za kisiasa zilizosababisha afungwe gerezani akiwa mfungwa namba 219. “Muziki sikuuchagua, bali ulinichagua, nikafanya kweli na dunia ikanijua, nilichofanya kwa hili gemu mnakijua. Mbeya ndiyo inanitesa (wanaitaka Mbeya), najua Mbeya ndiyo inanitesa. Lakini bado napenda Mbeya inavyonitesa,” inasema sehemu ya kiba