- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS : SIKU YA KIMATAIFA YA QUDUS KUFANYIKA NAIROBI NCHINI KENYA
Wapenda haki na amani nchini Kenya watajiunga na wenzao kote duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Quds Ijumaa wiki hii.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati Andalizi ya Siku ya Kimataifa ya Quds (Jerusalem) nchini Kenya, mjumuiko huo utafanyika katika Ukumbi wa Sir Ali Muslim Club Ijumaa kuanzia saa tisa Alasiri na kuhutubiwa na wanaharakati kadhaa wa kijamii na kisiasa.
Hali kadhalika kutakuwa na maonyesho ya filamu, picha, nyimbo na mashairi kuhusu kadhia ya Quds na baada ya hapo dhifa ya futari.
Taarifa hiyo imekumbusha kuwa, Siku ya Kimataifa ya Quds haina mfungamano wa kidini bali ni mjumuiko wa kisiasa unaowaleta pamoja Waislamu na wasiokuwa Waislamu ambao wanapinga ukoloni wa miaka 70 wa utawala wa Israel ambao unakalia kwa mabavu ardhi za Palestina na kuwakandamiza Wapalestina wanaopigania ukombozi wa ardhi zao. Halikadhalika taarifa hiyo imesema Siku ya Kimataifa ya Quds kwa ujumla ni siku ya wanyonge na waliodhulumiwa kuonyesha azma yao ya kupambana na madola ya kibeberu sambamba na kuunga mkono ukombozi wa wale wote wanaodhulumiwa duniani.
Miongoni mwa watakazozungumza katika mjumuiko wa Siku ya Kimataifa ya Quds mjini Nairobi ni Booker Ngesa Omole wa Chama cha Social Democratic cha Kenya, na Abdulqadir Nasser wa Harakati ya Mshikamano wa Kenya na Palestina.
Ikumbukwe kuwa kufuatia ubunifu wa Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds. Katika siku hii Waislamu na wapenda haki kote duniani hujumuika ili kubainisha kuchukizwa kwao na sera za kibaguzi za utawala wa Kizayuni wa Israel huku wakitangaza kuunga mkono malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina. Wapalestina wanapigania ukombozi wao kwa lengo la kuunda nchini huru ya Palestina, mji wake mkuu ukiwa ni Quds Tukufu.
Mwaka huu tarehe 8 Juni sawa na 23 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani itakuwa Siku ya Kimataifa ya Quds