Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 9:59 pm

News: Shirika la vijana na maendeleo Duniani latoa elimu kwa vijana Mkoani Dodoma

Dodoma: Shirika la vijana na maendeleo Duniani [SDG'S] leo machi 25 kwa kuungana na vijana wote Duniani wamefanya mkutano katika ukumbi wa African Dream uliopo maeneo ya royal mjini Dodoma. lengo ni kuhamasisha ajira, fursa kwa vijana na malengo endelemu ya Dunia [SDG'S].

Amani Shayo ni Rais wa shirika la vijana [AIESEC] Tanzania amesema lengo la mkutano huo nikuwaelemisha vijana ili waweze kuwa viongozi, kujikwamuwa kiuchumi, nakuwa wabunifu lakini amesema waliweza kukusanya maoni 2031 kwa vijana tofautitofauti hapa duniani.

Haya ni baadhi ya malengo ya maendeleo Endelevu ambayo wamejajadili.

1.Kufuta umasikini wenye sura zote kila mahali

2.kuondoa njaa, kuwa na Usalama wa chakula, kuboresha hali ya lishe na kukuza kilimo endelevu.

3.kuhakikisha maisha yenye siha njema na kuboresha ustawi kwa rika zote .

4.Kuhakikisha kuna elimu bora inayotolewa kwa usawa na kutengeneza fursa za kujiendeleza kwa wote.

5.kufikia usawa kwa jinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana.

6.kuhakikisha maji yanakuwepo, menejimeti yake na usafi inakuwa endelevu kwa wote.

7.Kuhakikisha kunakuwepo na chanzo rahisi cha kuaminika na endelevu cha nishati ya kisasa kwa wote.

8.kuboresha nakukuza uchumi endelevu wenye kutoa ajira na kazistaha kwa wote.

9.kuchenga miundombinu imara, kuanzisha viwanda endelevu, kufanikisha na kusukuma mbele ubunifu.

10.kupunguza pengo la umasikini ndani na miongoni mwa mataifa.

11.kuweka miji na makazi ya binadamu salama na yenye maendeleo endelevu.

12.kuhakikisha kunauwepo urari na ulaji na uzalishaji endelevu.

13.kuchukua hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na athari zake.

14.kuhifadhi na kuitumia bahari kwa maendeleo endelevu.

15.kulinda, kuanzisha nakuboresha matumizi endelevu ya mifumo ya ikolojia, kwa kufanya menejimeti ya misitu, kukabili majangwa, kuzuia upotevu na upotevu na uharibifu wa ardhi na kudhibiti kutoweka kwa bayaanuawai.

16.kujenga jamii kwa ajili ya maendeleo endelevu, haki kwa wote na kujenga taasisi zinazowajibika katika ngazi zote.

17.kuimarisha mfumo wa utekelezajiwa malengo na kufufua ushirikiano wa kimataifa katika kuleta maendeleo endelevu.