- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SHERIA KUTAMBUA DODOMA MAKAO MAKUU.
DODOMA: Wajumbe wa baraza la Ushauri la Mkoa (RCC) mkoani hapa, wametakiwa kutoa maoni na mapendekezo yao katika kufanikisha mchakato wa hatua ya kutungwa kwa sheria ya kuitambua Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.
Akifungua Mkutano huo jana Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Bilinith Mahenge alisema mkutano huo una lengo la kukusanya maoni ya mchakato wa hatua za kutungwa kwa sheria hiyo.
Dk.Mahenge alisema mkutano huo ni fursa kwa wajumbe wa baraza la Mkoa wa Dodoma ambao ni wenyeji wa makao makuu kutoa maoni hayo lakini wakitanguliza maslahi ya mkoa na Taifa badala ya kuangalia maslahi yao binafsi
Pia mkutano huo uliwashirikisha Wakuu wa Wilaya ,Wakurungenzi wa halmashauri,Wenyeviti wa Halmashauri ,Wakuu wa Idara wa Mkoa pamoja na Watalaamu kutoka Ofisi ya Rais-Tamisemi.
Alisema maoni hayo yanakusanywa ili baadaye itungwe sheria ambayo haikuwepo awali hapa nchini hata wakati makao makuu yalipokuwa Dar es Salaam, jambo ambalo lilichangia kukwamisha mchakato kuhamia Dodoma kwa miaka 45 tangu wazo lilipotolewa mwaka 1973.
Hata hivyo alisema maoni yao yatachangia kutungwa kwa sheria hiyo ambayo utekelezaji wake utakapoanza, utakuwa na manufaa kwao kutokana na mkoa kutambuliwa rasmi kuwa makao makuu nchi na hivyo kupewa kipaumbele katika mipango ya maendeleo.
Aidha alisema awali suala la kuhamia Dodoma lilisuasua kutokana na kutegemea utashi wa kiongozi wa kisiasa aliyepo madarakani, ndiyo maana miaka 45 ilipita bila utekelezaji wake kukamilika.
Aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli imeanzisha mchato wa kutungwa kwa sheria mpya ya kutambua makao makuu ambayo imeanza kupitia hatua mbalimbali kabla ya kupelekwa Bungeni .
Alisema kutokana na kutokuwapo kwa sheria hiyo, baadhi ya wizara au watendaji walihamia Dodoma halafu baada ya muda fulani wakarudi Dar es Salaam, hivyo kuwapo kwa sheria kutasaidia kusimamia mpango huo kikamilifu.
Katika mpango huo wa hatua za maoni hayo yakitolewa na kuafikiwa mapendekezo ya kutungwa sheria, kutakuwa na mafanikio makuba yakiwamo ya halmashauri zote za mkoa kuingizwa kwenye sheria hiyo na hivyo kuwa na nafasi sawa na kwenye uwekezaji na miradi ya maendeleo.
“Na hapa napenda kuipongeza Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli kwa kutekeleza wazo la kuhamia Dodoma ambalo limekwama kwa muda mrefu lakini pia kwa kuweka misingi ya kutunga sheria kwa ajili ya kutambua Dodoma kuwa makao makuu ya nchi’alisema Dk.Mahenge
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Rais-Tamisemi, John Cheyo alisema mchakato huo tayari wameshapokea maoni kutoka wizara mbalimbali ili kuweza kupata mapendekezo kwa kila maeneo mhimu
Hata hivyo Cheyo alisema mchakato wa hatua ya kukusanya maoni na mapendekezo ukikamilika katika baraza hilo yatapelekwa kwenye sekretariati ya baraza la mawaziri na kwa kamati ya ktaalamu na hatimaye mbele ya baraza la mawaziri ambalo ndilo lenye kuruhusu sheria itungwe au isitungwe.
Alisema mchakato wa kutunga sheria hiyo ulianza mwaka 2014 chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu lakini ulihusu kuiboresha Mamlaka ya Ustawishaji Makao makuu (CDA) ambayo kutokana na kuvunjwa kwake Mei 15 mwaka jana, wajibu huo umehamishiwa ofisi ya Tamisemi.
Aliongeza kuwa lengo la sheria hiyo ni kuboresha baadhi ya vipengere kwa sababu wazo la kuhamia serikali Dodoma, ilianzishwa wakati wa utawala wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K Nyerere mwaka 1973, lakini kutokana na kutokuwapo kwa sheria ya kutambua Dodoma kama makao makuu, utekelezaji umechelewa kwa miaka 45 hadi Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli ambayo inatekeleza.