November 29, 2024, 9:48 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI YATAMBUA MACHIFU NA MILA ZA TANZANIA.
BUNGENI DOM: Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amesema kuwa serikali inawatambua, machifu wa mila za Tanzania na ndiyo maana hata katika shughuli za kiserikali huwa wanashirikishwa huku akitolea mfano shughuli za mbio za mwenge. Shonza ametoka kauli hiyo mapema leo katika Kikao cha 48, Mkutano wa 11 kipindi cha maswali na majibu ambacho kinaendelea jijini Dodoma alipokuwa akiju swali la la Mbunge Taska Restuta Mbogo kwamba "Ni lini serikali itawatambua, Machifu na Watemi wa makabila mbalimbali ili waweze kusaidia kurekebisha maadili katika jamii za kitanzania?
Shonza amesema kwamba "Serikali inawatambua na itazidi kuwatambua watemi na machifu kwa kuwa ni njia moja wapo ya kuenzi na kudumisha mila pamoja utamaduni".
Akiongeza majibu ya swali hilo, Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Harisson Mwakyembe amesema kuwa wiki iliyopita alifanikiwa kuhudhuria katika maadhimisho ya kituo cha kumbukumbu ya utamaduni wa Kabila la Wasukuma huko Bujora Mwanza, ambapo Machifu wa wengi wa Kisukuma walihudhuria ambapo yeye alipata bahati ya kutunukiwa cheo cha 'Manji Mkuu wa ngoma', na kuongeza kuwa "nafasi ya machifu ni suala ambalo linaangaliwa kwa makini ili kuleta mjadala mpana ikiwa pamoja na kutambua nafasi zao kisheria".

Newest Posts