- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SERIKALI ITAENDELEA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATAALAM WA AFYA .
DODOMA: Serikali itaendelea kutoa kipaumbele kwenye sekta ya afya hususan swala la kuajiri wataalam wa kada mbalimbali za afya nchini kwa kuzingatia maeneo yenye uhaba mkubwa wa watumishi hasa maeneo ya vijijini.
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kuzindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi yaliyojengwa kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Maralia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mhe. Majaliwa ameendelea kusema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kutekeleza Malengo Endelevu ya Milenia hususan lengo nambari tatu linalohusu kuboresha afya za watu pamoja na ustawi wao.
“Miongoni mwa hatua hizo ni kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote ili kuongeza idada ya wataalam wa afya nchini kwa kuvijengea uwezo wa kimiundombinu vyuo vya elimu ya afya nchini ili viweze kuongeza udahili na kuzalisha wataalam bora wa afya” amesema Mhe. Majaliwa.
Aidha, Mhe. Majaliwa amewataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza idadi ya watumishi wa afya nchini watakaotekeleza majukumu yao kwa uadilifu na weredi mkubwa kwani Taifa bora linajengwa na wananchi wenye afya bora na afya bora kwa wananchi itapatikana iwapo watahudumiwa ipasavyo.
Mbali na hayo Mhe. Majaliwa alisema kuwa nchi bado inakabiliwa na changamoto ya magonjwa ya Kifua kikuu na Malaria ,hata hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya nchini imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za ugunduzi wa magonjwa hayo kwa kutumia vipimo vya vina saba (gene -expert).
“Tumefanikiwa kusambaza mashine za “gene expert” 191 kwenye Hospitali zote za Rufaa za Kanda ,Mikoa,Wilaya na baadhi ya vituo vikubwa vya afya ili kuwezeza kupata majibu ya vipimo vya utambuzi wa kifua kikuu ndani ya masaa mawili badala ya kipimo cha hadumini kinachotoa majibu baada ya masaa 24” amesema Mhe. Majaliwa
Aidha , Mhe. Majaliwa amewataka wananchi kujikinga na maambukizi ya Malaria kwa kuzuia mazalia ya mbu kupitia usafi wa mazingira wanayoishi na kutumia vyandarua kwa usahihi ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Kwa uapnde Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto mhe. Ummy Mwalimu ametoa shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutoa kipaumbele kikubwa katika masuala ya afya za Watanzania.
“Serikali kupitia Wizara yangu itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta ya afya yenye lengo la kuboresha huduma za afya na vyuo vya kutolea mafunzo ya kada za afya ili kuimarisha afya za wananchi” amesema waziri Ummy.
Naye Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za jamii Bw. Peter Maduki amesema kuwa mradi wa ukarabati ,upanuzi na ujenzi wa majengo mapya pamoja na vifaa tiba na tahama ulioanza April 2015 katika chuo hicho umegharimu shilingi Bilioni 5.2 ikiwa na malengo ya kuongeza uzalishaji wa wataalam wa afya nchini.