Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 7:29 pm

NEWS: SERIKALI IMEZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUZIWEZESHA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA.

JIJINI DODOMA: Serikali imezindua mpango mkakati wa kuziwezesha mamlaka za serikali za mitaa kutekeleza miradi yenye kuchochea upatikanaji wa mapato ili ziweze kujitegemea ambapo kwa kuanza imetenga shilingi bilioni 131.47 kwa ajili ya kutekeleza miradi 22 ya kimkakati katika halmashauri 17 hapa nchini.

Halmashauri hizo ni za mikoa kumi ya Dar es Salaam,Simiyu,Geita,Pwani Kigoma,Kilimanjaro,Songwe,Morogoro Lindi na Mtwara.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma na naibu waziri wa fedha na mipango Dk Ashtu Kijaji ambapo amesema kuwa baadhi ya halmashauri ya zinahitaji msukumo wa kati na wa ziada ili kuzisaidia kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka serikali kuu hivyo mkakati huo utazielekeza halmashauri kujielekeza kwenye miradi yenye tija kwa halmashauri na wananchi.

Awali katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango Doto James katika bajeti ya mwaka 2018/19 serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 131.47 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ikiwemo masoko ya kisasa,stand za mabasi na malori na kwamba halmashauri 17 zinazopata fedha hizo zilikidhi vigezo vya mkakati.

Hata hivyo tayari halmsahauri zimesaini makubaliano kati ya halmshauri na wizara kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa miradi mkakati.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Seleman Jafo amewataka wakurugenzi kusimamia kwa karibu miradi hiyo.

Mkakati huo umezingatia malengo ya dira ya maendeleo ya taifa 2025 pamoja na mpango wa pili wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano 2016/2017-2020/2021