Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 2:07 am

News; Serikali imeshindwa kuthibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite.

Dodoma; SERIKALI imesema kuwa nchi imeshindwa kudhibiti suala la utoroshwaji wa madini aina ya Tanzanite na hivyo kuwataka watendaji kusimamia kanuni na sheria katika kudhibiti wizi huo.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo.

Aidha aliwataka wafanyakazi kuwa wabunifu ili kuweza kuvumbua madini mapya pamoja na teknolojia mpya,ikiwemo ya kuchakata Madini kwa lengo la kuvutia wawekezaji.

Hata hivyo Waziri Muhongo amelitaka Shirika la umeme nchini (TANESCO)kwakushirikiana na wakala wa nishati ya umeme vijijini (REA)kuhakikisha bei ya umeme na gesi zinakuwa rafiki kwa wananchi ili kuepuka suala la uharibifu wa mazingira.