Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 1:46 am

NEWS: SERIKALI HUKUSANYA MRAHABA WA ZAIDI YA SH. BILIONI 175.5

BUNGENI DODOMA: Imeelezwa kuwa Katika kipindi cha kuanzia mwezi julai mwaka jana hadi mwezi march mwaka huu,jumla ya kilogram 30,953.59 za dhahabu zimezalishwa na migodi mikubwa na ya kati ya hapa nchini na kusafirishwa nje ya nchi huku wachimbaji wadogo wa madini hayo wakizalisha kilogram 2,021.4.

Uzalishaji wa madini hayo pamoja na madini ya almasi,Tanzanite na madini mengine umeiwezesha serikali kukusanya mrahaba wa zaidi ya shilingi bilioni 175.5.

Hayo yameelezwa na Waziri wa madini Angela Kairuki wakati akiwasilisha bajeti wa wizara hiyo leo jijini Dodoma.

kairuki amesema Katika kipindi hicho kiasi cha karati 248,083 za almasi zilizalishwa katika mgodi wa Mwadui huku zaidi ya kilogramu 535.9 za tanzanite zikizalishwa.

Hata hivyo amesema Madini hayo pamoja na madini mengine yaliyozaliswa katika kipindi hicho yameiwezesha serikali kupata mrahaba wa zaidi ya shilingi bilioni 175.5.

Aidha katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali ilikusanya maduhuli ya zaidi ya shilingi bilioni 225 sawa na asilimia 115 ya lengo lililopangwa na bunge ya kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 194.6.

Pamoja na kuvuka lengo la makusanyo ya maduhuli,kamati ya bunge ya nishati na madini hairidhishwi na kasi ya uendelezaji wa wachimbaji wadogo wanaotoa mchango mkubwa wa pato la serikali.

Katika mwaka wa 2017,sekta ya madini ilikuwa kwa asilimia 17.5 ikilinganishwa na asilimia 11.5 ya mwaka 2016 ongezeko hilo linatokana na uimarishwaji na udhibiti wa biashara haramu ya utoroshwaji wa madini.

Mbunge linaendelea jijini dodoma leo kikiwa ni kikao cha arobaini na moja