- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAWALIPA PENSHENI WAASTAFU 57,605
Waziri wa Fedha nchini Tanzania Dk. Philip Mpango amesema kuwa serekali imelipa mafao na pensheni kwa wastaafu wa Serikali 57,605, mirathi kwa warithi 1,006 na malipo ya kiinua mgongo kwa watumishi 457 wa Serikali walio kwenye mikataba,malipo haya yamefanyika kati ya Julai 2019 na Machi, 2020
Dk. Mpango ametoa taarifa hiyo leo15 Mei, 2020 Ijumaa Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara yake ya mwaka 2020/21. Amesema wizara inawajibika kulipa mafao na pensheni kwa watumishi wa umma ambao hawachangii katika mifuko ya hifadhi ya jamii, mirathi na malipo ya kiinua mgongo kwa watumishi wa Serikali walio katika mikataba na viongozi wa kisiasa.
Dk. Mpango amesema, wizara imeendelea kufanya uhakiki wa Daftari la Pensheni kila mwezi kabla ya malipo; kuandaa vitambulisho vipya vya wastaafu vya kielektroniki katika mfumo wa “smart cards” na kuboresha Mfumo wa unaotumika kutoa huduma kwa njia ya mtandao na kudhibiti fedha za mirathi zinazotoka Hazina kwenda moja kwa moja kwenye akaunti za warithi (Tanzania Pensioners Payment System – TPPS)