Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 1:45 am

NEWS: SEREKALI YATAKA KUPITTISHA SHERIA YA KUJIPIMA UKIMWI NYUMBANI

Dodoma: Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu amesema Wizara imemwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi ili kubadili sheria itakayo muwezesha kila raia kuweze kujipima Ukimwi nyumbani mwenyewe.

Akiongea leo Mei 31 bungeni wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mtambulie (CUF), Masoud Abdalla Salim ambaye ameuliza mkakati wa ziada wa Serikali kutambua wanaopata athari za Ukimwi. “Nchi nyingine wanatumia mate kutambua waathirika wa VVU (Virusi vya Ukimwi), Serikali ina mkakati gani wa ziada kutambua wale wanaopata athari za VVU hasa tukianza na Mkoa wa Dodoma.”ameuliza Salim Akijibu swali hilo, Waziri Ummy ambaye pia ana dhamana ya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto amesema sheria imekuwa kikwazo kwa wananchi kujipima maambukizi ya Ukimwi.

Mwanasheria mkuu wa Serekali Dkt. Adelardus Kilangi

Waziri Mwalimu amesema, ni kweli maambukizi yameongezeka kwa mkoa wa Dodoma kutoka asilimia 2.4 hadi asilimia 5 sawa sawa na mkoa wa Tanga na Mwanza. “Tunafanya utafiti maalumu kubaini kwa nini maambukizi yamepanda.

Tumekuwa na changamoto ya kuwapata wanaume kupima na njia ya mtu kujipima mwenyewe,” amesema Waziri Mwalimu Kuhusu dawa za VVU, Waziri Mwalimu amesema, zipo kwa asilimia 100. “Ukimwi si sentensi ya kifo, ukibainika tunakuingiza katika mpango wa kupata dawa.” amesema