- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAMKINGIA KIFUA RAIS MAGUFULI SWALA LA UJAUZITO SHULENI
Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha amefafanua kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hakuwahi kukataza waanafunzi waliopata mimba kuzuiwa kuendelea na masomo na badala yake alisisitiza kilichoamuliwa tangu 2002 kwenye serekali ya awamu ya tatu
Akitoa ufafanuzi wa jambo hilo leo bungeni wakati alipokuwa akimjibu mbunge Suzan Lymo ambaye alikuwa akitaka majibu ya namna serikali ilivyojipanga kuhusu zile sababu zilizo nje ya uwezo wa wanafunzi kuhimili kubeba mimba zinapatiwa ufumbuzi ikiwa tayari kuna tamko la kuzuia wanafunzi wasiendelee na shule lililotolewa na Rais Magufuli 2017.
Akijibu swali hilo Mh. Ole Nasha amesema kwamba Serikali imefanya marekebisho ya sheria ya elimu sura 363 ambapo imeongeza kipengele cha mtu yoyote ambaye atamuweka ujauzito mwanafunzi atafungwa miaka 30.
Mh. Nasha amesisitiza kuwa "Naomba nimsahihishe Mh. Lymo kwamba katazo lilikuwepo tangu 2012. Rais hajakataza wanafunzi waliopata ujauzito kutokuendelea na masomo. Alichokifanya ni kusisitiza kitu ambacho kilishaamuliwa siku nyingi." - Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha.
Aidha ameongeza kwamba "Serikali imeamua kuchukua uamuzi wa kuwazuia wanafunzi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni kuendelea na masomo, kwa lengo la kuwalinda, kwani wanaporejea shuleni hunyanyapaliwa na wenzao jambo ambalo huwaathiri kisaikolojia".
"Tunataka kuweka wazi kwamba, hatutegemei wanafunzi wetu katika umri mdogo waendelee kufanya mapenzi wakiwa mashuleni, kwa sababu inawaathiri katika masomo yao. Tumeamua kuchagua hatutaki kuchanganya mapenzi na elimu katika umri huo mdogo." ameongeza