- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAJIVUNIA KUINGIZA 77% YA WANAFUZI KIDATO CHA 5
Dar es salaam: Serekali ya Tanzania imeonyesha furaha kubwa kuwezesha wanafunzi wengi waliofaulu kidato cha 4 kujiunga na kidato cha Tano kwa mwaka wa 2018/2019,
Wanafunzi 70,904 kati ya 92,712 wenye sifa sawa na asilimia 76.5, wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, Vyuo vya Ufundi na Vyuo vya Elimu Kati kwa mwaka 2018 huku wanafunzi 21,808 wakikosa nafasi.
Hivi karibuni, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) lilitangaza matokeo ya Kidato cha Nne ambapo watahiniwa 95,337 sawa na asilimia 30 ya watahiniwa 317,777 waliofanya mtihani mwaka 2017 walipata daraja la I-III.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amewaeleza waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, kati ya hao, wasichana ni 31,884 na wavulana ni 39,020.
Amesema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2018 ni 58,927 ambapo kati yao wasichana ni 26,882 na wavulana 32,045.
“Kati ya waliochaguliwa, wanafunzi 30,317 wakiwemo wasichana 11,505 na wavulana 18,812 sawa na asilimia 51.4, watajiunga kusoma masomo ya tahasusi za sayansi na hisabati huku wanafunzi 28,610 wakiwemo wasichana 15,377 na wavulana 13,233 sawa na asilimia 48,6, wamechaguliwa kusoma tahasusi za masomo ya sanaa na biashara," alisema. Aliongeza,
"Wanafunzi 48 kati ya waliochaguliwa wana mahitaji maalumu wakiwemo wasichana 14 na wavulana 34 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano.”
Matokeo ya wanafunzi waliohitimu kidato cha nne mwaka 2016 na kufaulu kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa ajili ya mwaka jana, kati ya wanafunzi 96,018 wenye sifa, ni wanafunzi 93,019 sawa na asilimia 96.9 ndio waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi kwa kuwa walifaulu vigezo vyote vya msingi.
Kwa takwimu hizo, mwaka huu wamechaguliwa wachache ikilinganishwa na na mwaka jana lakini wakiwa juu ya mwaka 2016 ambapo jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana 31,700 walichaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.
Aidha, Jafo amesema shule 354 zikiwemo shule tisa mpya zimepangiwa wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu.
Kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi mwaka 2018, Jafo amesema wanafunzi 885 wakiwemo wasichana 173 na wavulana 712 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya ufundi ambavyo ni Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo cha Usimamizi wa Maendeleo ya Maji (WDMI) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST). Jafo alisema wanafunzi 11,977 wakiwamo wasichana 5,002 na wavulana 6,975 waliochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali katika ngazi ya Astashahada ya awali, Astashahada na Stashahada katika vyuo vya Elimu Kati vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) mwaka 2018.
Wanafunzi 2,525 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya afya, 4,697 vyuo vya ualimu, 440 (kilimo), 464 (ardhi Tabora na Morogoro), 2,850 (Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo) na 1,000 (Chuo cha Taifa cha Utalii).
chanzo Habari leo