Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 2:57 am

NEWS: SEREKALI YAFUTA EKARI 121,032 ZA ARIDHI

Serekali ya Tanzania imefuta umiliki wa Ardhi wa jumla ya ekari 121,032.2 za mashamba na kurejeshwa kwa wananchi baada ya kukiuka masharti ya uendelezaji.

Hii ni Katika usimamizi wa masharti ya umiliki na uendelezaji ardhi nchini.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameyasema hayo leo Mei 11, 2020 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Waziri Lukuvi amesema katika kuwezesha ulipaji wa fidia nchini, Wizara imeidhinisha jumla ya taarifa za uthamini wa kawaida 52,645, uthamini wa fidia na mali 84,223 na fidia 9,881 ya miradi mikubwa ya Kitaifa ya kimkakati.

Pia kupitia programu ya Funguka kwa Waziri, jumla ya migogo 15,808 ya ardhi imetatuliwa kiutawala katika Halmashauri mbalimbali nchini na migogoro 131,603 imetatuliwa kupitia Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya.