- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Sarafu ya Tanzania yamporomoka kwa asilimi 15 (Gavana BoT afunguka)
Dar es salaam: Hali ya kuporomoka kwa sarafu ya Tanzania imefanya kuwashtua baadhi ya wachumi ambao wanasema huenda ikatokea mfumuko wa bei. Wakati hali ikiwa hivyo mijadala mizito imeibuka katika mitandao ya kijamii mbalimbali kuhusu kuporoka huko kwa Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani.
Kwa sasa katika maduka mbalimbali ya kubadilishia fedha, jijini Dar es Salaam Dola moja ya Marekani inanunuliwa kwa kati ya Sh 2,270 na Sh 2, 290 kutoka Sh 2,180 mwanzoni mwa Januari mwaka huu.
Kwa mara ya mwisho katika miaka ya karibuni, shilingi iliporomoka zaidi Juni mwaka 2015 ambapo Dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa Sh 2,400 na baada ya BoT kuingilia kati ilishuka na kufikia Sh 1,967.
“Sisi kazi yetu ni kujaribu kutafuta utulivu (wa soko la fedha), kuna mambo yanasababishwa na ya nje, kuna mambo ambayo tunaweza kufanya sisi, hivi ninavyokueleza nia yetu ni kuhakikisha panautulivu na tunachukua hatua kwa madhumuni hayo,” alisema.
Alipoulizwa athari za kushuka kwa shilingi, Prof. Ndulu, alisema. “Hiki kitu kimetokea kwa muda mfupi hapa, tunajua namna tunavyotaka kudhibiti kwa hiyo kama itakaa kwa muda mfupi athari sijui kama zitakuwepo kwa hiyo subirini tufanye hiyo kazi,” alisema .
Alisema kwa sasa wanafanya juhudi za kuleta utulivu kutokana na mporomoko huo wa shilingi dhidi ya Dola ya Marekani huku akikataa kueleza mikakati hiyo kwa undani kwa sababu za kiufundi.
“Siyo kuuondoa (ushukaji wa shilingi) ni kwamba tutafanya juhudi zile zinataka kuleta utulivu, ndiyo kazi yetu, sasa tunafanya nini haswa hapa, hiyo itakuja kutuharibia shughuli yetu tusifanye sawasawa, hatufanyii magazetini,” alisema.
Alipomwuliza hatua ya kupanda huko kwa dola kama kunaweza kuathiri deni la Taifa la nje na la ndani, Profesa Ndulu alisema kama haijafika tarehe ya kulipa hayawezi kutokea madhara ya aina yoyote ila kwa siku husika ya malipo ndiyo inaweza kuwa hivyo kama dola itabaki kama ilivyo sasa.
“Sikia hii valuation (hesabu) unaweza kuifanya siku yoyote lakini madhara yake kama kutokea yanatokea unalipa, kama haijafikia tarehe ya kulipa itakupaje madhara? Labda tarehe ya kulipa haitakuwa (dola) huko juu itakuwa iko chini ndiyo ukweli,” alisem Profesa Ndulu