Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:33 pm

NEWS: SAKATA LA KUPIMA SAMAKI KWA RULA LAMTAFUNA WAZIRI MPINA

Dodoma: Sakata linalotikisa kwa sasa kwenye anga ya kisasa nchini Tanzania la maofisa wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi juzi kuingia ndani ya mgahawa wa Bunge na kupima kwa rula samaki waliopikwa limemgeukia Waziri wa Wizara hiyo, Luhaga Mpina, na kuonekana anafanya mambo ya kuabisha na kuchekesha, hivyo kulazimisha kuomba radhi mbele ya Bunge kwa Tukio hilo.

Hatua hiyo imemfanya Spika wa Bunge, Job Ndugai, Jana June 20, 2018 kusimama na kumpongeza waziri huyo, lakini akamweleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, namna ambavyo Bunge limesikitishwa na kitendo hicho.

Sambamba na hilo, Ndugai amesema Mpina anapaswa kujipima kwa alilofanya na mabunge mengine yakisikia waziri amefanya kitendo hicho, ni dharau ya hali ya juu kwa Bunge la Tanzania. Ndugai alsiema hayo baada ya Waziri Mpina kuliomba radhi Bunge na kukiri kwamba aliwaagiza maofisa hao kwenda kuwapima samaki hao. "Hata panapokuwa na kosa la jinai linafanyika katika eneo la Bunge, RPC (Kamanda wa Polisi Mkoa) anapaswa kunifahamisha na sisi si kazi yetu kulinda jinai.

Sisi hatulindi wahalifu, lakini lazima tuarifiane," alisema. "Mtu anaponunua samaki kilo 100 kwa akili ya kawaida, watu wananunua samaki kwa kilo si kwa futi.

Halafu samaki mwenyewe ameshakuwa kitoweo, sasa hii sheria ya kupima vitoweo itabidi tuzisome vizuri. "Hivi tunataka watu wafunge milango ndiyo wale samaki? Yaani samaki mbichi aliyevuliwa atafika Dodoma kwa muda gani, afanyiwe 'process' (utayarishaji) bado urefu wake huo huo wakati ameshapikwa? "Halafu wapimaji wenyewe wanapima mikono haina hata gloves (mipira ya kuvaa mikononi) wanapima, wanashikashika samaki na wamealika waandishi wa habari, wamejaa zaidi ya 20 kwenye chumba kimoja na baada ya pale wamerusha kwenye mitandao kama kuliweka Bunge mahali pasipostahili.

"Kwa kawaida ukikasirishwa sana na jambo, lazima usamehe kwa hiyo naomba waheshimiwa wabunge, tusamehe." Hata hivyo, kiongozi huyo wa Bunge amewataka wabunge kuwasamehe wahusika, akieleza kuwa pale kunapotokea jambo linakera na kukasirisha kwa kiwango kikubwa, ni vyema kusamehe.

KAULI YA MPINA Katika maelezo yake, Mpina alikiri kuwa ndiye aliyewaambia maofisa hao kufuatilia samaki aina ya sato wanaouzwa kwenye mgahawa huo kama wanakidhi vigezo vya kuvuliwa vya kuwa na urefu unaozidi sentimeta 25. "Nikamwagiza katibu wangu 'katika uhakiki unaoendelea, wakaguzi wajiridhishe katika Mgahawa wa Bunge' ambapo walibaini baadhi ya samaki ni wachanga waliokuwa na urefu chini ya sentimeta 25," Mpina alisema wakati akiwasilisha taarifa ya serikali bungeni kuhusu suala hilo jana.