- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SABABU ZA MNYIKA KUTOLEWA BUNGENI NA SPIKA
Dodoma: Mbunge wa Kibamba (CHADEMA) John Mnyika Jana Mai 9 alitolewa njee ya Bunge na Naibu Spika Tulia Ackson kwa kile kinachojulikana kuwa kutokuheshimu kiti cha spika wakati wa uchangiaji kwenye bajeti ya maji 2018/19, naye Mnyika muda mfupi baadae alitolea ufafnuzi swala hilo na kupinga kauli ya Naibu spika huyo na kusema kuwa sababu kubwa ya yeye kutolewa njee ya bunge ni kiti kutokuheshimu kanuni za bunge.
Mnyika ambae pia ni Naibu Katibu mkuu Bara siku ya Jumanne Mai 8 alitaka bajeti ya Wizara ya maji ya mwaka wa fedha 2018/19 isipitishwe kwanza mpaka Serikali iongeze kutoa fedha katika miradi ya maji zilizopitisha kwenye bajeti inayomalizika ya 2017/2018 ndipo jana akaitaka serekali itoe ufafanuzi Juu ya Hoja hiyo.
''Mpaka mwezi Machi serikali ilikuwa imetoa asilimia 22 tu kwenye bajeti ya maendeleo ya maji. Na asilimia 12.3 tu kwenye miradi ya umwagiliaji. Aidha, nilieleza kusudio la kutaka kuundwe kamati teule kuchunguza ufisadi kwenye miradi ya maji ambayo mingi inayotajwa kukamilika maji hayatoki na kuna matumizi mabaya" alisema Mnyika
sasa Jana baada ya Waziri wa Fedha kwenye hotuba yake kutokueleza kabisa hoja ya Mnyika ya sababu ya serikali kushindwa kutoa fedha za ndani kama zilivyopitishwa na Bunge kwenye miradi ya maji wakati ikitumia fedha taslimu kununua ndege na matumizi mengine yaliyo nje ya bajeti, ndipo mbunge huyo alisimama ili kutoa hoja kwa majibu wa kanuni ya 69
''Naibu Spika alinipa nafasi ya kuisoma kanuni ya 69(1) inayosema "mbunge anayependa mjadala unaoendelea juu ya hoja yoyote uahirishwe hadi wakati wa baadaye, anaweza kutoa hoja 'kwamba mjadala sasa uahirishwe' na atataja mjadala huo uahirishwe hadi wakati gani na pia atalazimika kutoa sababu kwanini anataka mjadala uahirishwe. Badala" kiti kuheshimu kanuni " hiyo na kunipa nafasi ya kueleza sababu na kutaja tarehe, Naibu Spika akatumia vibaya kanuni 69(2) kukataa hoja hiyo nisiiwasilishe na kurusu Wizara ya maji ihitimishe mjadala ili bajeti ya Wizara ya Maji ipitishwe. Niliposimama kutaka kanuni zifuatwe ndipo Naibu Spika alipoagiza nitoke nje." alisema Mnyika
Mnyika aliongeza kuwa "Hii ilikuwa mara ya pili kwa "kiti kutokuheshimu kanuni" siku ya leo dhidi yangu. Awali nilitaka taarifa ya upande mmoja ya Serikali iliyotolewa na Waziri na Waziri Mkuu kuhusu uhaba wa mafuta ya kula na kupandishwa kwa bei ijadiliwe na Bunge, lakini Naibu Spika alikataa kinyume cha kanuni"