- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Sababu za DC wa Magufuli kuachia Ngazi
Tabora:
Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Gabriel Mnyele amedaiwa kuachia ngazi bila kutoa sababu za uamuzi huo na jana aliwaaga madiwani wa CCM wilayani humo katika kikao kilichofanyika kwenye ofisi za chama hicho.
Hata hivyo, licha ya baadhi ya madiwani kuthibitisha, mwenyewe alipotafutwa baadaye kwa simu, alidai kuwa hajaachia ukuu wa wilaya, ila amewaaga kuwa anakwenda Dar es Salaam huku akisema kwamba mamlaka ya uteuzi ndiyo inayopaswa kuzungumzia suala hilo.
Lakini, kwa mujibu wa madiwani hao akiwamo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Uyui, Said Ntahondi, mkuu huyo wa wilaya aliingia katika kikao chao na walipompokea kama Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa Wilaya kwa wadhifa wake, aliwaeleza kuwa yeye si Mkuu wa Wilaya ya Uyui tena na kwamba alikuwa amemwandikia Rais John Magufuli kumuomba apumzike wadhifa huo. Hata hivyo, hakueleza sababu.
Ntahondi alisema Mnyele aliwaaga jana alasiri na kuwaleza kuwa alimuomba Rais Magufuli amkubalie kuachia nafasi hiyo aliyoishikilia kwa muda usiozidi miezi minane.
Alipotafutwa kwa simu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri alisema, “Jaribu kumtafuta yeye mwenyewe (Mnyele) azungumzie suala hilo.”
Pia, Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Mussa Iyombe alipoulizwa kuhusu uamuzi huo wa Mnyele alisema,
“Sifahamu kwa kweli kuhusu suala hilo, nilikuwa kwenye kikao ndiyo namaliza muda huu (12:36 jioni), nitafuatilia nitakachopata nitakufahamisha.”
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene alisema, “Sina taarifa rasmi, nasikia kama unavyosikia wewe.”