November 23, 2024, 2:37 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Saa chache zimebaki Trump kuapishwa waandamanaji wafunga mitaa
Washington: Donald Trump atakuwa rais wa 45 wa Marekani amerejelea ahadi yake ya kampeni ya kuifanya nchi yake kuwa taifa lenye nguvu zaidi kuliko hapo awali, Hata hivyo maelfu waandamana nchini Marekani kupinga kuapishwa kwake
Trump anatarajiwa kuapishwa wakati ambapo nchi yake imegawanyika vibaya. Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni, ni asilimia 40 tu ya Wamarekani ndio wanamuunga mkono. Hata ambapo maalfu ya watu wanaomuunga mkono wanatarajiwa kumshamngilia bilionea huyo aliyejigeuza kuwa mtetezi wa maslahi ya tabaka la wafanyakazi, maalfu kwa maalfu ya Wamerakani wengine wanatarajiwa kwenda Washington kuzipinga sera zake wakati wa kuapishwa kwake.
Licha ya hayo makamu wa rais mteule, Mike Pence, amesisitiza kwamba Trump yupo tayari kuanza kazi: Trump ataapishwa na Jaji Mkuu John Roberts wa Mahakama ya Juu ya Marekani. Marais watatu wa zamani pamoja na waheshimiwa wengine kadhaa, ikiwa pamoja na aliyekuwa mpinzani wake mkuu kwenye uchaguzi wa Novemba mwaka jana, Bi Hillary Clinton, watahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Trump.Lakini thuluthi moja ya wabunge wa chama cha Democratic wataisusia hafla hiyo. Maalfu ya wapinzani wa Trump waliandamana jana mjini New York wakiwemo wacheza filamu maarufu Robert de Niro, Alec Baldwin na muongoza filamu mshindi wa tuzo ya Oscar, Michael Moore, wakipinga siasa za Trump kuelekea wahamiaji, Waislamu na huduma za afya na kijamii. Kilele cha shughuli za leo kitafikiwa kwa hotuba ya Trump kwa Wamarekani, mara baada ya kula kiapo cha kuingia madarakani. Msemaji wake, Sean Spicer, amesema kwamba hotuba yake ya kuingia ikulu haitakuwa juu ya ajenda anazotaka kuzitekeleza, bali zaidi itakuwa ya kifalsafa jinsi anavyoiona Marekani. Spicer pia amesemaTrump yupo tayari kuzitekeleza sera zake mara tu atakapoanza kazi ikiwa pamoja na kutia saini hati zinazohusu huduma ya afya, ugaidi na uhamiaji.