- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Rungu jipya lawashukia viongozi wa umma, Kairuki asema "Hakuna atakae baki"
Dar es salaam; Ikiwa siku chache zimepita Baada ya serikali kufanya tendo la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma pamoja na wafanyakazi hewa na yote hayo ikiwa lengo kuifanya tanzania ya viwanda na kukuza uchumi wa wawatanzania. waziri wa nchi ofisi ya rais menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora , Angellah Kairuki amesema serikali imetenga fedha katika bajeti ya mwaka 2017/18 kwa ajili ya uhakiki wa mali za viongozi .
Kairuki alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mfumo wa kielektroni wa menejimeti ya taarifa za kimaadili , alisema ifikapo Desemba 31, viongozi wa umma watajaza fomu za maadili kwa njia ya mtandao.
Desemba, mwaka jana sekretarieti ilipanga kuhakiki mali za viongozi 500, lakini walifanikiwa kuhakiki mali za viongozi 15,824 wanaotakiwa kuhakikiwa nchi nzima ili kukidhi matakwa ya kisheria
hata hivyo jana sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma ilisema imeshindwa kuhakiki mali za viongozi hao 384 kwa sababu imekosa fedha za kutosha kutekeleza jukumu hilo la kisheria .
Naye kamishina wa maadili Jaiji Harold Nsekela alisema mfumo huo utatumika kuhifadhi taarifa za viongozi wa umma na malalamiko ya wananchi.
Alisema viongozi wengi bado hawajahojiwa kwa sababu idadi yao ni kubwa na sekretarieti haina fedha za kutosha kuhakiki taarifa zao.
Hata hivyo amewaomba viongozi kutoa taarifa sahihi kuhusu mali na madeni wanayodaiwa