- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RIPOTI YA MAABARA YA TAIFA YABAINI MADUDU
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema Ripoti ya Uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii imebaini kuwepo kwa Mojawapo ya Mashine za kupima sampuli za Covid-19 ilikua na hitilafu bila Uongozi wa Maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati.
Waziri ummy amesema Leo Mei 23, 2020 kuwa Maabara hiyo ilikuwa inamapungufu makubwa kwenye mfumo wa uendeshaji wa kitaaluma na kuwepo na upungufu wa wataalam wanaoendana na Maabara hiyo.
" Ripoti imebaini mapungufu katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya COVID-19" amesema Ummy Mwalimu.
“Maabara hii mpya ina uwezo wa kupima sampuli 1800 za ugonjwa wa Covid-19 ndani ya saa 24 tofauti na ile ya awali iliyokuwa na uwezo wa kupima sampuli 300 tu” amesema Bi Mwalimu
"Imebainika kuwepo kwa upungufu wa wataalamu wenye sifa za mafunzo ya Bio-technology na Molecular Biology katika sekta ya Afya ikiwemo katika maabara kuu ya Taifa" amesema Waziri Ummy.
HATUA ZILIZOCHUKULIWA BAADA YA KUBAINI ‘MADUDU’ MAABARA YA TAIFA YA AFYA YA JAMII
"Hivi sasa upimaji wa sampuli zote za Covid-19 umehamishiwa katika maabara mpya iliyokamilika kujengwa katika eneo la Mabibo Dar es Salaam ambayo kwa sasa ndiyo itakuwa maabara ya Taifa.
Wizara imeelekeza kuanza kutumika kwa mashine nyingine zilizoko katika maabara mpya iliyopo Mabibo Dar es Salaam ambazo zilikuwa zimeagizwa na zimewasili nchini.
Wizara imeshaanza kurekebisha mfumo wa utawala, utendaji na kitaaluma ndani ya maabara hii" - Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya.