Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 1:36 pm

NEWS : RIPOTI INAONYESHA UJASUSI NCHINI MAREKANI UMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 300

Tovuti ya taasisi inayopinga vita ya Anti War imetoa ripoti na kueleza kuwa ujasusi unaofanywa na serikali ya Marekani kwa raia wa nchi hiyo umeongezeka kwa kiwango cha asilimia 300.

Image result for Anti War

Ripoti hiyo iliyotolewa kwa anuani ya "Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani lingali linaendelea kudukua mawasiliano ya simu ya Wamarekani" imebainisha kuwa katika mwaka uliopita wa 2017, serikali ya Marekani ilifuatilia na kusajili mawasiliano ya simu na ya jumbe za maandishi yapatayo nusu bilioni ya raia wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, takwimu hizo zinaonyesha kuwa kiwango hicho ni sawa na ongezeko la asilimia 300 ya ujasusi uliofanywa na serikali ya Washington dhidi ya raia wake kulinganisha na mwaka 2016.

Taasisi ya Anti War imeongeza kuwa ufuatiliaji na udukuaji huo wa taarifa binafsi za raia umefanywa kwa kutumia sheria ya uangalizi wa taarifa za nje iitwayo FISA.

Edward Snowden

Mwaka 2013, Edward Snowden, afisa wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani na mfichuaji maarufu wa taarifa za intelijinsia za shirika hilo alifichua na kuweka hadharani nyaraka nyingi za siri za mipango ya kijasusi ya serikali ya Washington zikiwemo zinazohusiana na sheria ya uangalizi wa taarifa za nje.

Maafisa wa serikali na wa vyombo vya usalama nchini Marekani wanaitumia vibaya sheria ya FISA ili kunasa taarifa kuhusiana na harakati za kawaida na za maisha ya kila siku ya mamilioni ya raia wa nchi hiyo na hata wale wa nchi za Ulaya