Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:55 pm

NEWS: RASMI TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI NA KAMPENI

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania(NEC) imetangaza rasmi ratiba ya Uchaguzi wa Rais na wabunge wa Jamhuri ya Muungano na madiwani wa Tanzania Bara.

Akizungumza leo Julai 22,2020 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa(mstaafu)Semistocles Kaijage amesema kwamba katika ratiba hiyo uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais, ubunge na udiwani itakuwa Agosti 25 mwaka huu na kampeni za uchaguzi zitaanza Agosti 26 hadi Oktoba 27 mwaka huu.

Amesema kwa mujibu wa ratiba hiyo ya NEC ni kwamba siku ya Uchaguzi itakuwa Oktoba 28 mwaka huu." Tume ya Taifa kwa mamlaka iliyopewa chini ya ibara ya 41(4) ya Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,ikisomwa pamoja na vifungu vya 35B(1),(37)(1)(a) na 46(1) vya sheria ya Taifa ya uchaguzi.

"Sura ya 343 na kifungu cha 48(1) cha sheria ya Serikali za mitaa ,sura ya 292 inapenda kuutarifu umma kuhusu ratiba ya uchahuzi mkuu,amesema Jaji Kaijage alipokuwa akianza kutoa ratiba hiyo ya uchaguzi."

Aidha tume hiyo haikutaka kuruhusu maswali kupeleka uchaguzi kuwa siku ambayo itakuwa ni katikati ya juma, licha ya wanahabari kujiandaa na maswali ya kuhoji zaidi. Itakumbukwa kuwa chaguzi zilizopita tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi takriban miongo miwili sasa, tanzania ilizoeeleka uchaguzi kufanyika jumapili ya mwisho wa mwezi wa kumi, hatua ilioleta mazoea miongoni mwa wananchi kuwa huenda hata uchaguzi wa mwaka huu ungelifanyika katika tarehe hizo.