November 24, 2024, 1:27 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Rais wa Misri atangaza hali ya Hatari baada ya shambulio Hili
Cairo: Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi ameamua kutangaza hali ya hatari nchini kote kwa muda wa Siku tatu, na hii inakuja kufuatia shambulizi la bomu ambalo limeua zaidi ya watu 40 katika makanisa mawili ya jamii ya Coptic.
El-Sisi ameliagiza Jeshi nchini Misr kusaidia polisi kulinda maeneo muhimu na vikosi vya usalama vitaruhusiwa kukatwa mtu bila kibali cha kukamatia.Kufuatia tukio hilo, Rais Sisi pia ametangaza kuundwa kwa baraza litakalopambana na ugaidi na watu wenye itikadi kali.
Mpaka sasa saa chache baadaye baada ya shambulio hilo Kundi la kigaidi la IS limekiri kuhusika kwenye shambulio hilo,Baadhi ya watu waliotoa maoni yao ni Bw Ahmed Abdel Hady mbaye ni muislamu anasema kuwa kamwe shambulio hilo halitaweza kuwagawa Wamisri.