- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA KOREA AKUBALI OMBI LA TRUMP KUZURU MAREKANI
Kiongozi wa taifa la Korea kaskazini Kim Jong Un amekubali mwaliko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuitembelea Washington baaada ya mkutano wa kihistoria baina ya mataifa hayo mawili nchini Singapore Jumanne, Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini limeripoti.
Kim pia alimwalika pia Trump kutembelea Pyongyang.
"Viongozi hao wawili wakuu walikubali mwaliko wa kila mmoja," shirika la KCNA limeripoti.
Baada ya mkutano wa saa kadhaa, rais Trump na Kim Jong Un, walitia saini mkataba wa maelewano, kikubwa kikiwa ni kukubali kwa Korea Kaskazini kuachana kabisa na mradi wake wa kutengeneza silaha za nyuklia.
Kitu kingine kilichokubaliwa, ni kwa Marekani kusitisha mazoezi ya kijeshi na Korea Kusini, mazoezi ambayo kwa muda mrefu Korea Kusini imekuwa ikisema ni uchokozi.
Kim Jong Un amesema, ameepuka vikwazo vingi kukutana na rais wa Marekani huku Trump akisema, anaamini kuwa Korea Kaskazini itaanza kutekeleza mpango wa kuachana na mradi wake wa nyuklia mara moja, huku akiahidi kuwa Marekani itahakikisha kuwa Korea Kaskazini inakuwa salama.
Hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanaoana kuwa makubaliano hayo hayana uzito kwa sababu hayajaelezea ni vipi Korea Kaskazini itaacha kutekeleza mradi wake wa nyuklia, lakini rais Trump amefafanua kuwa Marekani itatuma wawakilishi wake kuthibitisha hilo.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesifu makubaliano hayo na kusema kukutana kwa viongozi hao wawili, kutaandika historia mpya ya amani kati ya nchi yake na Korea Kaskazini.
Wachanganuzi wanasema kuwa ni nafasi nzuri ya kuendeleza uhusiano baina ya nchi mbili, lakini wakosoaji wanasema kuwa hii huenda ikasababisha majaribio ya mapinduzi ya serikali Korea kaskazini.
Hakuna tarehe iliyotolewa kwa ziara hiyo lakini katika mahojiano na shirika la habari la Fox News, Trump alikuwa amesema baadaye kwamba Kim anakaribishwa kuzuru White House wakati wowote ule utakaofaa.
Hayo yakijiri, Marekani imewahakikishia washirika wake katika eneo la Asia Mashariki kwamba itatekeleza majukumu yake ya kuwalinda.
Hii ni baada ya Rais Trump kukubali kufutilia mbali mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini baada ya kukutana na Bw Kim.
Korea Kaskazini imekuwa ikiitaka Marekani kusitisha mazoezi hayo yanayofanyika kila mwaka kwa muda mrefu