- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS WA CHINA KUZULU NCHINI RWANDA
Raisi wa China Xi Jinping anaanza rasmi ziara yake ya siku mbili nchini Rwanda,ikiwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa taifa hilo kuzuru nchini Rwanda.
Serikali ya Rwanda imesema ziara ya kiongozi wa China ni muhimu na imelenga kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.
Kwa mujibu wa waziri wa masuala ya kigeni wa Rwanda Olivier Nduhungirehe Xi Jinping na raisi wa Rwanda Paul Kagame watasaini mikataba 15 kabla kiongozi huyo kutamatisha ziara yake jumatatu.
Waziri Nduhungirehe amesema mataifa hayo mawili yatasaini pia makubaliano ya Jiolojia,upanuzi wa hospitali ya Masaka,ujenzi wa barabara na uwanja wa ndege wa Bugesera.
Aidha Xi atafanya mazungumzo na raisi Paul Kagame na badae kuzungumza na vyombo vya habari.
Kiongozi huyo wa china atatembelea pia eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari mjini kigali na baadae kukutana na jumuiya ya wachina wanaoishi nchini Rwanda.