- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS SHEIN AFANYA UTEUZI WA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR
Zanzibar: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, amemteua Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
Katika taarifa iliyotolewa leo Juni 20, 2018 na Ofisi ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, imesema Rais Dkt. Shein, amefanya uteuzi huo chini ya kifungu 119 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Pia Rais Dkt. Shein amefanya uteuzi wa wajumbe wengine sita wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ambao ni Mabruki Jabu Makame, Feteh Saad Mgeni na Makame Juma Pandu, wengine ni Dkt. Kombo Khamis Hassan, Jaji Khamis Ramadhani Abdula na Bi Jokha Khamis Makame.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa wajumbe wote walioteuliwa wanatakiwa kufika Ikulu ya Zanzibar, Ijumaa Juni 22, 2018 saa 4:00 asubuhi kwaajili ya kuapishwa.
April 18, 2018 aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha alitangaza kustaafu baada ya kumaliza muda wake kama mwenyekiti wa tume hiyo baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano tangu April 30, 2013.