- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS MKAPA AFARIKI DUNIA USIKU WA LEO
Aliyekuwa Rais wa serikali ya awamu ya tatu nchini Tanzania Benjamin William Mkapa amefariki dunia akiwa na miaka 81.
Kifo hicho kimetangazwa usiku wa kuamkia leo Julai 24, 2020 na Rais wa sasa wa nchi hiyo John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli ametangaza kupitia runinga ya taifa taarifa za kufariki dunia kwa kiongozi huyo wa awamu ya tatu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
''Mzee Benjamin William Mkapa Rais wa awamu ya tatu amefariki. Amefariki kwenye hospitali mjini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa. Niwaombe watanzania tulipokee hili. Taifa limepata msiba mkubwa. Tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele ya haki," ametangaza rais Magufuli.
Taarifa hiyo hata hivyo haikuweka wazi Mzee Mkapa alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani.
Rais Magufuli tayari ameshatangaza siku saba za maombolezo kufuatia kifo hicho.
Katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Twitter rais Magufuli amemuomboleza Mkapa na kusema atamkumbuka "kwa mapenzi yake makubwa kwa Taifa, ucha Mungu, uchapakazi na utendaji wake katika kujenga uchumi."
Mzee Mkapa alizaliwa Novemba 1938, Mkoani Mtwara kusini mwa Tanzania, na aliliongoza taifa hilo kwa mihula miwili toka mwaka 1995 mpaka 2005.