- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Rais Magufuli amfuta kazi Waziri Nape Nnauye
Dar es salaam: Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la mawaziri ambapo aliye kuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Harrison Mwakyembe atakuwa Waziri wa Habari sanaa Utamaduni na Michezo, Katika nafasi ya Mwakyembe Rais Amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Hatua ya Nape kuondolewa kwenye nafasi yake inakuja siku chache baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kuvamia kituoa cha Clouds Media Group,
ambapo Nape kama waziri mwenye dhamani aliunda kamati ya Uchunguzi kufuatilia kama ni kweli Makonda alivamia kituo hicho, Na baada ya saa 28 kamti ilimkabidhi Nape ripoti hiyo iliyo kiri kuwa Pasipo na shaka Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alivamia kituo hicho na kutaka kurushwa kwa kipindi chake, ambacho kilikuwa kina mama mmoja alie dai kuwa amezaa na Askofu wa kanisa la ufufuo na Uzima Dr Askofu Josephat Gwajima.