Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 7:45 pm

NEWS: RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Dar es salaam: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Mohammed Ali Ahmed kuwa Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Visiwani Zanzibar.

Kupitia Taarifa iliyotolewa Leo June 20, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Mohammed Ali Ahmed umeanza leo tarehe 20 Juni, 2018.

Kabla ya uteuzi huo Bw. Mohammed Ali Ahmed alikuwa mwanasheria na mtafiti katika Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar.

Bw. Mohammed Ali Ahmed amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rajab Baraka Juma ambaye amestaafu.