- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIS KENYATTA ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO KUFUATIA KIFO CHA RAIS MKAPA
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa Taifa la Kenya itakuwa katika maombolezo ya siku tatu baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.
Maombolezo hayo kitaifa yatakuwa kuanzia siku ya Jumatatu mpaka Jumatano.
Bendera nchini humo na ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti kwa siku tatu za maombolezo.
Benjamin Mkapa alikuwa na mchango mkubwa kwa Kenya katika masuala mbalimbali hasa ya kidiplomasia, akiwa mmoja kati ya watu muhimu walioshiriki mchakato wa kupatikana kwa amani nchini Kenya wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya za mwaka 2008.
Viongozi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania wametoa salamu za rambirambi kwa Watanzania na Rais John Magufuli kutokana na kifo cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa.