- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RAIA WA UGANDA KUTOZWA KODI KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII
Serikali ya Uganda yapitisha muswanda tata wa kuwatoza kodi watumiaji wa mitandano ya kijamii na huduma za miamala ya kifedha kwa njia ya simu.
kila mtu anayetumia mitandao kama vile facebook, WhatsApp Viber na Twitter anatakiwa kulipa shillingi mia mbili za nchi hiyo kiwango ambacho wananchi wanasema ni kikubwa mno ukilinganisha na kipato chao kwa siku.
Wananchi wa Uganda wameendelea kuilalamikia sana upitishwaji wa sheria hiyo ambayo wanahisi inawanyima haki ya kufanya mawasiliano.
Rais Museveni alisisitiza kuhusu muswada huo akidai kuwa mabadiliko ni muhimu na kwamba mitandao ya kijamii imekuwa ya kwanza kusambaza umbea na habari zisizokuwa na uhakika.
Akihojiwa Jana , Monica Amoding, ambaye ni mmoja wa wabunge wa chama tawala cha NRM amesema anapinga kupitishwa kwa muswada huu.
Sheria hiyo inatakiwa kuanza kutekelezwa ifikapo Julay 1. lakini kabla ya hapo tayari kumeanza kuwa na mashaka juu ya utekelezwaji wake.