- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Professa Gabriel awataka maafisa wa mawasilino kushirikiana na waandishi wa Habari
Dodoma; Naibu katibu wizara ya habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo professa Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Katibu Mkuu kiongozi engine John Kijazi amefunga kikao kazi cha maafisa mawasiliano serikalini ambapo ufungaji huo umefanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma kikao hicho kilianza machi 13 na kufungwa tarehe 17 machi mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo professa Gariel amesema Kutokana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi anawasihi chama cha maafisa mawasiliano serikali [TAGCO] washirikiane na vyombo vya habari katika kufanikisha utoaji wa taarifa za serikali kwa umma .
Vilevile ameweza kuwapongeza wadhamini wote ambao ni TCRA,EU,NSSF,PPF,SSRA,TSN,TANAPA,TFDA,TAGCO,UONGOZI INSTITUTE,WCF,PSPF,TTCL,na PUSH OBSERVER Nakusema kuwa waendelee kushirikiana ili kuendelea kuletea mafanikio katika jamii na watumishi wa umma.