November 23, 2024, 5:00 pm
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Pombe aina ya togwa yauwa mmoja , tisa wanusurika kufa
Serengeti ; watu tisa wanusurika kufa na mmoja aliyetajwa kwa jina la Marwa Sinda miaka [5] amefariki dunia wilayani Serengeti mkoani Mara baada ya kunywa pombe ya kiyenyeji aina ya togwa.
Kaimu mganga wa hospital teule ya Nyerere wilayani serengeti Richard Majahazi amethibisha kupokelewa kwa wagonjwa waliodawa kunywa pombe hiyo ambapo Marwa Sinda amefariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini hapo
Naye ofisa mtendaji wa kata ya kisangura Maria Mwangomo amesema watu hao wamekunywa pombe hiyo nyumbani kwa Daniel Sinda mtaa wa wa kisangura ambapo mama wafamilia hiyo Sophia Sinda na watoto wake watatu ni miongoni mwa waliodhurika kwa kunywa togwa