- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: POLISI YATOA ONYO KWA WANAOTAKA KUMPOKEA LISSU
Jeshi la Polisi nchini limewaonya vikali watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kuhamasisha wananchi wengine kukusanyika kinyume cha sheria kwasababu ya kwenda kumpokea Makamu mwenyekiti wa chadema Tundu Lissu na hivyo kuagiza kuacha mara moja tabia hiyo la sivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza siku ya Julai 27 mwaka huu ni siku ya kwenda kumpokea Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya chama hicho, Tundu Lissu ambaye amekuwa nje ya nchi tangu Septemba 7, 2017.
Onyo hilo limetolewa na Msemaji wa Jeshi hilo, SACP David Misime amesema wamefuatilia nchi nzima kuona kama kuna taarifa iliyofikishwa katika kituo cha polisi kwa ajili ya mkusanyiko huo lakini hawakukuta taarifa yoyote.
“Tumeona katika mitandao ya kijamii baadhi ya viongozi wa Chadema wakihamasisha wananchi kukusanyika kutoka maeneo mbalimbali ya nchi Julai 27, ili kumpokea kiongozi mmoja wa chama hicho anayetarajiwa kurejea nchini.
“Kurejea kwake ni haki yake kama ilivyo kwa Watanzania wengine kwasababu nchi yetu iko salama sana kwa maisha ya Watanzania hata kwa wageni wanaofika nchini na kukusanyika ni haki ya kila Mtanzania lakini hakuna haki isiyokuwa na wajibu kwa mujibu wa sheria za nchi,” amesema SACP Misime.