Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 8:25 pm

News: Onyo kali latolewa na serikali kwa waliovamia msitu wa kibindu

Bagamoyo: Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais [muungano na mazingira] January Makamba ametoa lai kwa wananchi wa kata ya kibindu wilayani Bagamoyo juu ya wananchi waliovamia msitu huo nakuweka makazi katika hifadhi hiyo kinyume cha sheria lazima waondoke na hatua zitachukuliwa zidi yao.

Makamba ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara alipotembelea msitu huo uliopo kata ya kibindu katika Halimashauri ya Mji Mdogo wa Chalinze mkoa wa Pwani nakuwasisitiza wananchi kuwa waliovamia lazima waondoke katika eneo hilo ili kuhifadhi na kulinda msitu ziguo ambao ni miongoni mwa vyanzo vya maji katika mto wami.

''Eneo hili tutatumia sheria mbili za mazingira na misitu amabayo inasema mtu akiingia kwenye hifadhi ya misitu na kufanya shughuli za kibinadamu ni kosa la jinai na anaweza kufungwa''.

''Naomba muwapelekee salaamu wenzenu walioweka makazi waambieni tutawashtaki na kuwapeleka mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake'',alisema Makamba.