Home | Terms & Conditions | Help

November 30, 2024, 3:50 pm

NEWS: OFISI ZA MABASI YA MWENDOKASI KUHAMISHIWA UBUNGO

Dar es salaam: Uwongozi wa Halimashauri ya Jiji la Dar es Salaam unafanya mazungumzo ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo kasi (Udart), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo(UBT).

Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana Mai 8, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika kutokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika magari hayo.

Isaya Mwita,

Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo waweze kufikia mwafaka.

“Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,” alisema Mwita.

Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini.

Meya alisema jambo hilo linaweza kupunguza mafuriko katika eneo la Jangwani na maeneo karibu na mto huo.

Tokeo la picha la jangwani mabasi ya mwendokasi

Alisema fedha za upanuzi huo zimekwisha kutolewa, kilichobaki ni utekelezaji wa mradi kuanzia daraja la Salendar hadi Pugu.

“Awamu ya kwanza ya mradi itaanzia Salendar hadi Kigogo, jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo la mafuriko kwa wakazi wa Jangwani na maeneo jirani ya mto Msimbazi,” alisema.