- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: OBAMA ALAANI VIONGOZI KUTUMIA UBABE BADALA YA DEMOKRASIA
Aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama amesema enzi hizi ni za watawala walio na ubabe na kwamba demokrasia ya sasa haitiliwi uzito sana.
Ameyasema hayo kwenye Umati wa watu 15,000 Jana July 17 akihutubu katika mhadhara wa kila mwaka wa Nelson Mandela nchini Afrika Kusini ambao huandaliwa kila mwaka kama sehemu ya maadhimisho ya kukumbuka kuzaliwa kwa kiongozi huyo wa zamani wa Afrika Kusini.
Huku akionekana kumkosoa mrithi wake Donald trump, Bw Obama amesema watawala wenye nguvu wanahujumu karibu kila taasisi ya serikali ambayo huleta maana kwa demokrasia.
Bw Mandela alizaliwa 18 Julai mwaka 1918 na mwaka huu ni karne moja tangu kuzaliwa kwake.
Obama amesema kiongozi huyo aliyepambana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini alikuwa mtu shujaa kweli na anayefaa kukumbukwa katika historia.
Aidha Bw Obama amesema kuna kizazi kizima cha watu ambao wamekulia na kulelewa katika ulimwengu uliojaa uhuru zaidi na wa kuvumiliana.
"Hili linafaa kutupatia matumaini," ameongeza.
"Lakini ulimwengu unakabiliwa na tishio la kurejea katika mtindo wa zamani na hatari zaidi na katili wa kufanya mambo.
"Ni lazima tuanze kwa kukubali kwamba sheria zote ambazo huenda zilikuwepo kwenye vitabu …. Miundo ya zamani ya hadhi na mamlaka na unyanyasaji vyote viliangamizwa, lakini havikuangamizwa kabisa," amesema.