- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Nyumba za FFU Moshi zateketea kwa Moto
Kilimanjaro:
Moto mkubwa uliotokea jana usiku wilaya ya moshi mkoa wa Kilimanjaro ambapo moto huo ulianza majira ya saa 2:00 usiku ambao chanzo chake bado hakijafahamika,
moto huo umeteketeza jengo la ghorofa mbili la makazi ya Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) la mjini Moshi usiku wa kuamkia leo
Vikosi vya zimamoto na uokoaji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Kiwanda cha Sukari cha TPC vilikuwa vikiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Mashuhuda wame mwambia muakilishi wetu kuwa moto huo umeanza saa 2: na hadi kufikia saa 4:00 ulikuwa umeteketeza ghorofa ya pili unakosadikiwa kuanzia.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa familia zote za askari wa kikosi hicho cha FFU wanaoishi katika nyumba hiyo wamefanikiwa kutoka salama isipokuwa baadhi ya mali zimeteketea.
Wakazi wa kitongoji hicho wameshuhudia jitihada kubwa zikifanyika za kuuzima moto huo lakini unaonekana kuzidi kushika kasi baada ya gari la Halmashauri kuishiwa maji.
Hii ni mara ya pili kwa jengo hilo kuungua moto, miaka ya hivi karibuni lililipuka moto na vikosi vya zimamoto vilifanikiwa kuudhibiti.