- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NONDO AANDIKA BARUA YA KUMKATAA HAKIMU KWENYE KESI YAKE
Iringa: Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Tanzania na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo ameiandikia barua Mahakama ya Wilaya ya Iringa kumkataa hakimu John Mpitanjia anayesikiliza shauri lake.
Nondo amesema kuwa anamtilia mashaka Hakimu huyo hivyo ameandika barua hiyo ili mahaka itende haki
Wakili wa Nondo, Jebra Kambole ndiye aliyewasilisha barua hiyo ambayo imeeleza kuwa kuna mazingira yasiyo rafiki katika kesi hiyo.
Baada ya kuwasilisha malalamiko hayo, wakili wa Serikali, Abeid Mwanadalamo alidai kujiondoa kwa hakimu kutakubaliwa iwapo tu malalamiko yaliyoletwa ni ya msingi na ushahidi upo wazi. “Kama aliona kuna kasoro alitakiwa alete malalamiko yake mwanzoni si leo,” alieleza. Mwandalamo alieleza kuwa hizo ni njama za kutaka kuchelewesha shauri hilo na akaiomba mahakama kulitupilia mbali ombi hilo. Kambole alidai ni haki ya mshtakiwa kumkataa hakimu kama anaona haki haitendeki. Baada ya maelezo hayo, hakimu Mpitanjia aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 16 kwa ajili ya uamuzi