Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 9:50 pm

NEWS: NAPE AIPINGA SHERIA ALIYOPITISHA MWENYEWE BUNGENI

Dar es salaam: Aliyewahi kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye ameibuka Hadharani na kuonekana kukasirishwa na kitendo cha serikali kuanza kutumia sheria ya makosa ya Kimtandao kwa wale wote wanao chapisha maudhui kwenye mitandao, Sheria hiyo ya mtandao ambayo kimsingi kama utakumbuka Nape ndiye aliyekuwa kinara wa kuipitisha Bungeni.

kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter huku akiambatanisha picha ya mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo Nape amesema, “Hili la JF (Jamii Forum) linafikirisha.

"Ukizuia watu kusema wayawazayo unaweza kutana nao..... kimya kimya!." aliandika Mbunge huyo

Mmoja wa watu waliokomenti kwenye mbunge huyo, akiwemo Goodluck Mayani amesema, “Nimeona kwenye 'status' za watu hii taarifa inayohusu Jamii Forum nikasema ngoja kidogo nikimbie Twitter kwa habari zaidi, ghafla nakutana na hii tweet yako@Nape Moses Nnauye Naye Wilb-jr amesema, “yajayo yanafurahisha sana na tutaona mengi sana ila mheshimiwa ulikuwa sehemu ya kutungwa kwa sheria hizi ukiwa waziri leo hii inakuumaje kwa sheria husika kuanza kufanya kazi.

Wachapishaji wa maudhui katika blogu na majukwaa ya mtandaoni wanatakiwa kusajiliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kupata leseni kulingana na gharama zilizoanishwa. Baadhi ya mitandao imedai kusitisha huduma hizo kutokana na tangazo la TCRA linalosema ni kosa kisheria kutoa huduma ya maudhui ya mtandaoni bila kuwa na leseni, hivyo kuanzia Juni 11, 2018 watoa maudhui hawaruhusiwi kuweka taarifa mtandaoni.

Pia kanuni hizo zinaipa nguvu TCRA kudhibiti mawasiliano ya mtandaoni kwa kuchukua hatua kwa wasiotimiza wajibu ikiwamo kuamuru kuondolewa kwa ‘maudhui yasiyofaa’ na usajili wa watumiaji na majukwaa. Kanuni hzo zinatokana na Sheria ya Mawasiliano ya Kielekroniki na Posta ya mwaka 2018.