Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:34 pm

NEWS: NAPE AGOMA KUIUNGA MKONO CCM

Dodoma: Mbunge wa Mtama Nape Nnauye ambaye anatokea kusini mwatanzania ametamka wazi kuwa hayuko tayari kuunga mkono mabadiliko ya sheria ya matumizi ya fedha (financial Bill) iliyopelekwa Bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango kwa madai ya sheria hiyo kutaka kuhujumu pesa za Ruzuku ya wakulima wa korosho ya asilimia 65%

"Haya mabadiliko ya sheria ya matumizi ya fedha yaani, finace bill, hatuyaungi mkono mpaka pale ambapo bunge litakapofanya uamuzi," alisema Nape bada ya kuhojiwa na kituoa cha habari cha BBC

Kumekuwa na Mjadala mkali ukiendelea bungeni kuhusu mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2018 /2019 kuhusu zao la korosho. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuondolewa kwa ruzuku ya asilimia 65 iliyokuwa inaenda kwenye Mfuko wa Maendeleo wa Korosho na badala yake, iende kwenye mfuko mkuu wa serikali.

Mjadala huo, unaonekana kugusa zaidi hisia za wabunge hasa wa mikoa ya kusini ambao moja kwa moja wametoafikiana na mpango huo licha ya kuungwa mkono na Wengine kama Kina Zitto Kabwe, Hussein Bashe na wengineo. Wakati huo huo, hofu kubwa imetanda miongoni mwa wadau wa kilimo cha korosho hasa katika mikoa ya Kusini.