- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News; Naibu Spika Dk Tulia Ackson amejipanga kuboresha miundombinu sekta ya Elimu
Mbeya ; Kutokana na juhudi za serikali kujenga shule za sekondari katika kila kata lakini suala la uboreshaji bado linaendelea naye Naibu spika wa mbunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson amemwomba mkuu wa shule ya sekondari ya loleza Emily Fwambo mkoani Mbeya kuandaa tathimini ya ukarabati wa bweni na kuipeleka kwa Naibu spika wa Bunge , Dk Tulia Ackson.
Hata hivyo Dk Tulia amesema amejipanga kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu na afya kutokana na ukweli kwamba, ndizo nguzo muhimu katka maisha ya binadamu na zinagusa maisha ya wananchi wengi .
Naye mkuu wa shule ,amesema watafanya tathimini hiyo mapema iwezekanavyo.
''Tathmini nitaitoa mapema iwezekanavyo kwa kuwa mwaka jana Dk Tulia ulitusaidia kukarabati bweni moja na vyoo ambalo linatumiwa na wanafunzi zaidi ya 25 '',amesema Fwambo