- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: NAIBU SPIKA AMKINGIA KIFUA WAZIRI MKUU KUJIBU SWALI WARAKA WA KKKT
Dodoma: Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amemzuia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kujibu swali la Mbunge wa Mvunjo James Mbatia kuhusu Serikali kutoa siku 10 kwa Kanisa la Kiinjili la kiinjili Tanzania KKKT kufuta waraka wake wa pasaka walioutoa March 24 mwaka huu
Swali hilo limeulizwa katika kipindi cha Maswali ya papo hapo kwa Waziri Mkuu Leo June 7, 2018 Katika swali lake, Mbatia ametaka kujua ukweli kuhusu barua hizo . “Kuna barua wamepewa KKKT na TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ) wakitakiwa kufuta nyaraka zao za Kwaresima,” aliuliza Mbatia na kuitaka Serikali kueleza uamuzi huo una lengo gani?
lakini baada ya kumaliza kuuliza swali hilo, Dk Tulia amesema haliwezi kujibiwa na kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni
Mara baada ya swali hilo, naibu spika huyo amesema, “mtakumbuka mheshimiwa Kubenea (Saed-mbunge wa Ubungo-Chadema) alimuuliza waziri Mkuu swali linalohusu dini na mheshimiwa Spika alizuia suali hilo lisijibiwe.”
Baada ya maelezo hayo, Dk Tulia alimuita mbunge mwingine kuuliza swali huku Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi akiketi na kuzungumza na na wabunge wengine wa vyama vya upinzani chini kwa chini.
KKKT iliandikiwa barua ya kutakiwa kufuta waraka wao na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, limeulizwa leo Alhamisi Juni 7, 2018 katika kipindi cha Maswali ya papo hapo kwa Waziri Mkuu na mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia.