Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 6:40 pm

News: Mzozo wa umeme wazua gumzo kwa Rais Magufuli

Dar es salaam ; Ikiwa siku chache zimepita baada ya kaimu Mkurungezi Mkuu wa TANESCO jijini Dar es salaam kutoa siku kumi na nne za wadaiwa sugu kuhakikisha wamelipa madeni yao. sakata la deni la umeme la sh121 billioni ambalo tanesco inadai zanzibar , limechukua sura mpya baada ya wabunge na wawakilishi kutofautiliana kauli na kuonya hatari za kuibua kero mpya ya muungano.

Deni hilo lilizungumziwa na Rais John Magufuli alipokuwa mtwara hivi karibuni na kutaka Tanesco ikate umeme Zanzibar kutokana na kudaiwa kiasi hicho cha fedha.

kufuatia kauli hiyo ya Rais Magufuli Kaimu mkurungezi mkuu wa tanesco dk Tito Mwinuka juzi alitoa siku 14 kwa shirika la umeme zanzibar [zeco] kilipa deni hilo la sivyo watakatiwa umeme .

Hata hivyo Rais wa Zanzibar DK Ali Mohamed Shein Juzi jioni alisema iwapo Tanesco itakata umeme wataweza kurudia katika matumizi ya asili ambayo ni kutumia vibatari kupata mwanga.

kutokana na kauli hizo wabunge wawakilishi waliozungumza na muakilishi Media jana walisema jambo hilo siyo suala la kulipa tafsiri ya kisiasa au kero ya muungano.

Naye Mbunde wa kigoma mjini kupitia chama cha ACT -wazalendo, Zitto Kabwe alisema "Hili ni suala linalohitaji utatuzi kwa weledi wa hali ya juu".