Home | Terms & Conditions | Help

November 29, 2024, 5:39 pm

NEWS: MZEE MAJUTO ARUDI TANZANIA AHIDI KUACHANA NA UIGIZAJI

Dar es salaam: Muigizaji nguli nchini Tanzania, Amri Athuman maarufu Mzee Majuto ameahidi kuachana na sanaa ya kuigiza kama atafanikiwa kupona tena kwani kwa jinsi alivyoteseka hana hamu ya kuigiza tena ili apate muda mwingi wa kupumzika

Jana Ijumaa Mzee majuto aliwasili kutoka India baada ya kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi, India. Mzee Majuto alienda India kutibiwa tezi dume baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu, hata hivyo baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam amepelekwa katika Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupumzishwa kutokana na uchovu wa safari.

Akizungumza Leo June 23, 2018 Baada ya kuwasili Tanzania Majuto amesema anaendelea vizuri na anamshukuru Mungu pamoja na Rais John Magufuli kwa kuwezesha matibabu yake pamoja na Watanzania kwa ujumla wake.

“Nashukuru afya yangu inaendelea vizuri, namshukuru Rais Magufuli kwa kuwezesha safari yangu na matibabu ya kwenda kutibiwa India.

“Pia nawashukuru Watanzania wote kwa maombi yao, nawapenda sana ila naomba wazidi kuniombea ili nipone haraka na jambo langu la kuwaambia nikipona naacha kuigiza,” anasema Majuto. Mei 4 mwaka huu alisafirishwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu baada ya kuugua kwa takribani miezi mitatu.