- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MWILI WAKUTWA UMENING'INIA KWENYE KAMBA MBEYA
Mwili wa kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 23 na 25 umekutwa ukining'inia juu ya mti katika kata ya Isyesye jijini Mbeya akidaiwa kuwa amejinyonga kwa kutumia kamba na kusababisha taharuki kwa wananchi wanaishi kwenye eneo hilo.
Baadhi ya watu ambao wameshuhudia tukio hilo wamesema kuwa wameamka asubuhi ya leo na kushangaa kukuta mwili wa kijana huyo ambaye bado haujafahamika ukiwa unaning'inia juu ya mti na walipousogelea wakabaini kuwa mtu huyo ameshapoteza maisha ndipo wakaamua kutoa taarifa polisi huku wakiomba serikali kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha kifo hicho.
Kaimu mwenyekiti wa mtaa huo wa RRM Isyeye, Uswege Paulo Mwakalobo amesema hilo ni tukio la kwanza kutokea katika mtaa wake ambapo akawataka wananchi wanaofika kushuhudia tukio hilo wasisahahu kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa kutosababisha msongamano.
Licha ya askari wa jeshi la polisi kufika katika eneo la tukio na kuuondoa mwili wa marehemu, lakini kamanda wa polisi mkoa wa mbeya, kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi Ulrich Matei hakupatikana kuzungumzia tukio hilo.
#ITV