- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Mwigulu aligeukia Jeshi la Polisi ataka kuwa na Nidhamu na Maadili
Dodoma. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba amefungua mkutano na maafisa wakuu wa jeshi la polisi machi 27 Katika jengo la LAPF lililopo maeneo ya makole mjini Dodoma lengo la mkutano huo ni kutathimini na kujua maendeleo ya mwaka 2016 na namna ya utendaji wa kazi kwa mwaka 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari Nchemba amesema jambo la msingi ni kuimalisha Tanzania ya Viwanda ili kuinua uchumi na pia ameongeza kwa kusema wawekezaji hawezi kuja kuwekeza kama hakuna usalama nchi.
Nchemba ameweza kutaja sifa za askari polisi ni lazima awe na nidhamu na maadili katika utendaji wa kazi,
baadhi ya malalamiko ambayo ameyataja ni;
1. watu kubambikiziwa makosa,
2. watu kubadilishiwa kesi.
kauli mbiu ya mkutano huo ni ''zingatia maadili tunapopambana na uhalifu ili kuimarisha usalama kwa maendeleo ya taifa''