Home | Terms & Conditions | Help

November 23, 2024, 11:12 pm

News: Mwakyembe hayuko tayari kuchukua hatua Dhidi ya ripoti ya NAPE.

Dodoma:Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr, Harrison Mwakyembe amesema hayuko tayari kuchukua hatua yoyote kuhusiana na ripoti aliyoicha aliyekuwa waziri wa habari Nape Nnauye kabla ya kuenguliwa nyazifa hiyo kuhusiana na alichokifanya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mh. Poul Makonda kuvamia ofisi za Cloud media akiwa na timu ya watu wenyewe silaha[Bunduki].

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Katika jengo la LAPF mtaa wa makole mjini Dodoma wakati wa mapokezi na watumishi wa wizara hiyo Mwakyembe ametolea majibu swala hilo katika kipengele cha maswali na majibu ambapo swali hilo limeulizwa na mwandishi wa gazeti la mtanzani daima Danison Kaijage kuwa ''mtangulizi wako Nape Nnauye aliacha ripoti ya kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Poul Makonda ni Hatua gani Umeichukua mpaka sasa''.

mwakyembe amesema hayuko tayari kuchukulia hatua ripoti hiyo kwa sababu ambazo ni

Hizi ni sabau za Mwakyembe kuhusiana na Ripoti ya Nape Nnauye.

1.Kama mwanasheria hawezi kupeleka taarifa kwa Rais ambayo haijakamilika .

2. Ushahidi wa Makonda haupo hawezi kupeleka taarifa hiyo kutokana na kuheshimu kanuni na sheria za uandishi.

Lakini atakachokifanya ''Nitakaa na kamati yangu ili kujua chanzo cha swala hilo''.amesema Mwakyembe.