- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Mwakyembe Asisitiza Utamaduni kukuza lugha ya kiswahili.
Dodoma; Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na Michezo DR. Harrison Mwakyembe amesisitiza utamaduni utumike kukuza lugha ya kiswahili hapa nchi ili kiswahili kiweze kukuwa kwa kasi hapa duniani.
Mwakyembe Ameyasema hayo wakati akipokelewa katika ofisi za waziri mkuu jengo la LAPF Mtaa wa makole gorofa na nane mjini dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari nakutolea maelezo kipengele cha sekta ya utamaduni kuwa utumike katika kukuza lugha ya kiswahili hapa nchi nakusema hapa duniani kuna lugha elfu sita [6000] kati ya lugha hizo kiswahili kimeshika nafasi ya kumi duniani.
Mwakyembe ameongeza kuwa sera ya sanaa na sera ya filamu imepewa kipaumbele kwa sababu nimiongoni mwa sekta ambazo zinasaidia kukuza uchumi wa Tanzania nakuongeza kipato kwa jamii.lakini pia katika sekta ya michezo amesema.
''Napenda sana michezo lakini kinachonikatisha tamaa kila siku tiimu ya Tanzania taifa star kutokufanya vizuri katika michezo tofautitofauti hapa duniani'',amesema Mwakyembe.